• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

  Makabiliano kati ya raia katika wilaya mbalimbali Burkina Faso

  Mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya raia katika wilaya kadhaa nchini Burkina Faso wiki hii.

  Makabiliano hayo yaliyotokea ni kati ya wafuasi wa chama kimoja katika baadhi ya maeno na katika maeneo mengine ni wafuasi wa vyama mbalimbali vya kisiasa.

  Baada ya uchaguzi wa madiwani, ni wakati sasa wa uchaguzi wa waku wa wilaya. Hali ambayo imezua mvutano.

  Katika jimbo la Karangasso-Vigué, karibu kilomita 400 magharibi mwa mji mkuu, kiongozi mmoja aliyechaguliwa alishambuliwa na watu wanaopinga uchaguzi wake. kiongozi huyo amejeruhiwa na ameruhusiwa kulazwa katika hospitali ya Bobo-Dioulasso, mji wa pili wa nchi ya hiyo.

  Meya mpya wa manispaa ya Gomboro Moussa Diallo, magharibi mwa nchi, alipigwa mawe na waandamanaji.

  Majengo ya manispaa ya mji yameteketezwa kwa moto.

  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako