• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

  Jean-Pierre Bemba ahukumiwa kifungo cha miaka 18 jela

  Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC,, wamemuhukumu kifungo cha miaka 18 jela, aliyewahi kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC Jean-Pierre Bemba.

  Hukumu dhidi ya Bemba inatolewa ikiwa ni miezi michache imepita toka mahakama hiyo, imkute na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vya ubakaji vilivyotekelezwa na askari wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  Mwezi Machi mwaka huu mahakama ya ICC baada ya kusikiliza pande zote kwenye kesi husika, na baada ya Jean-Pierre Bemba mwenyewe kuomba radhi kutokana na yale yaliyotokea wakati akiwa kiongozi, bado ilimkuta na hatia.

  Jean-Pierre Bemba o alikamatwa na maofisa usalama wa Ubelgiji Mei 24 mwaka 2008, baada ya kutolewa kwa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake na alijisalimisha kwenye mahakama hiyo, Juni 3 mwaka 2008.

  Awali waendesha mashataka wa mahakam hiyo, waliiomba mahakama imuhukumu kifungo cha miaka isiyopungua 30 jela, kutokana na makosa yenyewe aliyokutwa nayo na hatia.

  Licha ya upande wa utetezi kudai kuwa mteja wao hakuhusika kwa vyovyote vile kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu, majaji wa mahakama hiyom walijiridhisha pasipo na shaka kuwa Bemba alishiriki kwenye kuamrisha askari wake kutekeleza uhalifu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako