• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

    (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47
    Abubakar Shekau asema bado ndiye kiongozi wa Boko Haram

    Kiongozi anayepigwa vita wa kundi la Boko Haram amesema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo licha ya taarifa ya kundi la Islamic State kwamba ameng'olewa mamlakani.

    Abubakar Shekau alipuuzilia mbali uamuzi wa IS kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa kundi hilo.

    Shekau amemshtumu al_Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.

    Kundi la Boko Haram linapigania kuipindua serikali ya Nigeria ili kutangaza serikali ya Kiislamu katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo.

    Katika kipindi cha miezi 18 iliopita,kundi hilo limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti baada ya kukabiliwa vilivyo na jeshi la Nigeria na majirani zake.

    Aidha wizara ya ulinzi ya Nigeria imepuuza taarifa za mabadiliko katika uongozi wa kundi la kigaidi lka Boko Haram.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo Rabe Abubakar imesema, mabadiliko hayo hayana umuhimu na hayana athari yoyote kwa operesheni ya kijeshi inayoendelea kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Amesema kwa sasa, askari wanajitahidi kuwaondoa wapiganaji waliobaki wa kundi hilo ambao wamezagaa kwenye eneo hilo.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako