• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

  (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47

  Chama cha ANC chaongoza katika matokeo ya kura nchini Afrika Kusini

  Msemaji wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Bw. Zizi Kodwa amesema, matokeo ya hivi karibuni yanaonesha kuwa chama hicho kinaongoza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

  Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa, ANC kilipata asilimia 54 ya kura zote, na chama cha upinzani cha umoja wa demokrasia DA kilipata asilimia 26 ya kura.

  Bw. Kodwa amesema, matokeo hayo yamethibitisha kuwa, wananchi wana imani na chama cha ANC kuendelea kuiongoza nchi hiyo kwa mara nyingine, na wamejitokeza nchi nzima kusisitiza tena ajenda za chama hicho za maendeleo, kupinga umasikini, na kuwahudumia wananchi wake.

  Chama cha Democratic Alliance, kimekuwa kikiungwa mkono na wazungu pamoja na chotara, japo wapiga kura weusi wameanza kukiunga mkono, kwa kukatishwa tamaa na mwendo wa kobe wa uimarishaji wa uchumi wa chama tawala cha ANC, na sakata nyingi zinazomkabili rais Jacob Zuma.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako