Mashindano ya Olimpik yaanza mjini Rio De Janeiro Brazil.
Mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 yamefunguliwa wiki hii mjini Rio De Janeiro Brazil.
Maelfu ya wachezaji mashabiki na wadau wa michezo wanaendelea kuwasili mjini humo kwa ajili ya mashindano hayo makubwa zaidi duniani .
Kumekuwa na kashfa kadhaa zinazorindima mashinano hayokama vile ukosefu wa usalama maji chafu kwenye bahari na maandalaizi duni.
Hata hivyo serikali imesema kila kitu kiko shwari na Brazil iko tayari kuendesha Olimpiki ya kipekee.
Timu ya kwanza ya olimpiki ya wakimbizi imefanya hafla ya kupandisha bendera katika Kijiji cha Olimpiki, hatua inayoonesha ujumbe wa moyo wa michezo kwa wakimbizi wote duniani.
Hii ni mara ya kwanza kwa wakimbizi kushiriki Olimpiki.
Kikosi hicho cha wakimbizi kina wanariadha watano kutoka Sudan Kusini, waogoleaji wawili kutoka Syria, wachezaji wawili wa judo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, mkimbiaji mmoja wa marathon kutoka Ethiopia, na makocha watano na maofisa wengine watano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |