• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

    (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47

    Burundi yalikataza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutuma kikosi nchini humo

    Serikali ya Burundi imekataa uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupeleka kikosi cha polisi nchini humo kusimamia hali ya usalama na haki za binadamu inayoendelea kuwa mbaya.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali ya Burundi Philippe Nzobonariba inasema, serikali ya nchi hiyo ilishangaa kusikia Baraza hilo limepitisha haraka azimio namba 2303 la kupeleka askari 228 nchini Burundi.

    Amesema uamuzi huo utakuwa na matokeo mabaya kwa nchi nyingine kwa sababu umetolewa bila idhini ya Burundi.

    Ameongeza kuwa, hali ya amani na usalama imeboreshwa na askari na wasimamizi 200 wa haki za binadamu wa Umoja wa Afrika watapelekwa nchini humo hivi karibuni kwa kuwa mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na Umoja wa Afrika yanaendelea.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako