• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

    (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47

    Rais wa Sudan Kusini awatimua mawaziri sita wa upinzani

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewatimua mawaziri sita kutoka chama cha upinzani cha SPLM-IO na manaibu wawili. Mawaziri hao waliotimuliwa kwenye taarifa ya kiserikali iliyotolewa kupitia hotuba ya Rais iliyotangazwa kwa njia ya televisheni ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani Bw Alfred Lado Gore.

    Hatua hiyo ya Rais imekuja baada ya aliyekuwa waziri wa kilimo Bw Lam Akol kujiuzulu na kutoa mwito wa kuwepo kwa mabadiliko ya serikali, na kusema makubaliano yaliyosainiwa kwa lengo ya kukomesha vita iliyodumu kwa miezi miwili yamekufa.

    Mawaziri hao sita waliofukuzwa ni wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzani cha SPLM IO Bw Riek Machar ambaye aliukimbia mji wa Juba baada ya kulipuka kwa mapambano makali kati ya wapiganaji wanaomtii na wale wanaomtii Rais Kiir.

    Wakati hayo yakijiri Msemaji wa Dkt Riek Machar ameonya kuwa huenda Sudan Kusini ikatumbukia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe iwapo Umoja wa Afrika hautaingilia kati.

    Bw Mabior Garang de Mabior amesema wanajeshi waaminifu kwa Dkt Machar wako tayari kuingia mji mkuu wa Juba iwapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halitaidhinisha pendekezo la Umoja wa Afrika la kutuma wanajeshi nchini humo.

    Haijabainika iwapo Dkt Machar, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Salva Kiir, ana wanajeshi wa kutosha wa kumuwezesha kujaribu kuingia Juba.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako