• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

    (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47

    Watu wa Zimbabwe waandamana kupinga mpango wa serikali kutoa noti mpya

    Mamia ya raia wa Zimbabwe wameandamana wiki hii na kupambana na polisi wakati wakipinga mpango wa serikali kuanzisha noti mpya za dhamana za serikali zenye thamani sawa na dola za kimarekani.

    Waandamanaji hao pia wametoa ombi kwa wizara ya fedha na kutaka serikali ifirikie kwa makani uamuzi huo.

    Baada ya kushuhudia mfumuko mbaya wa bei, serikali ya Zimbabwe mwezi Aprili mwaka 2009 ilitangaza kuacha kutumia sarafu yake na kuruhusu sarafu za aina tisa kutumiwa, na hivi sasa dola ya kimarekani ni sarafu kuu nchini humo.

    Hata hivyo uhaba wa dola unatokea kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa zinazoagizwa kwa wingi, urari mbaya wa biashara na uimara wa dola katika soko la kimataifa.

    Uamuzi huo wa kuanzisha noti mpya za dhamana ulifanywa kwa ajili ya kuzuia mtiririko wa kwenda nje wa dola na kuboresha hali ya mzunguko wa sarafu hiyo, lakini pia umesababisha hofu kwenye soko la fedha.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako