• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Julai-5 Agusti)

  (GMT+08:00) 2016-08-05 19:20:47

  Umoja wa Afrika watuma waangalizi nchini Zambia kufuatilia uchaguzi mkuu wa Agosti 11

  Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini-Zuma ameidhinisha kutuma waangalizi nchini Zambia kufuatilia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika Alhamisi wiki hii.

  Timu hiyo ni ya kwanza ya aina yake kutumwa na Umoja huo kwa kuwa inayowashirikisha wataalamu wa uchaguzi, sheria, siasa, vyombo vya habari, na kampeni.

  Wakati huo huo Rais wa Zambia, Edgar Lungu amesema yuko tayari kutumia mbinu zozote kuhakikisha kwamba nchi hiyo ina amani baada ya uchaguzi huo wa wiki ijayo wa rais, bunge , na serikali za mitaa pamoja na kura ya maoni.

  Lungu amesema kuwa ana ripoti za kijasusi kuwa wanachama wa chama kikuu cha upinzani , UPND, wanapanga kuzua vurugu iwapo chama chao hakitashinda katika uchaguzi huo.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako