• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 1-Oktoba 7)

    (GMT+08:00) 2016-10-08 17:18:59

    Kibunga chauwa watu 300 Haiti

    Wiki hii zaidi ya watu 300 wamefariki baada ya kibunga Matthew kukumba Haiti, hayo ni kwa mujibu wa serikali.

    Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka.

    Hadhi ya Kimbunga Matthew kwa mara nyingine imepandishwa hadi ngazi ya nne, hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbali mbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini Marekani.

    Maafisa wa serikali ya Haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na maafa yaliyosababisha na kimbunga hicho.

    Siku ya alhamisi, serikali ya nchi hiyo ilisema watu mia moja tayari walikuwa wamepoteza maisha yao.

    Kimbunga Matthew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Caribbean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.

    Wengi wa waliopoteza maisha nchini Haiti, walikuwa wakiishi mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi katika maeneo ya pwani ya kusini.

    Wengi walifariki baada ya kuangukiwa na miti, taka zilizokuwa zikisombwa au hata kusombwa na maji, baada ya mito nyingi kuvunja kingo zao.

    Kimbunga hicho kiliambatana na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya hadi kilomita 280 kwa saa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako