• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 1-Oktoba 7)

    (GMT+08:00) 2016-10-08 17:18:59

    Vikosi vya AMISOM vyawaua wapiganaji 7 wa kundi la Al-Shabaab kusini Somalia

    Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimesema kimewaua wapiganaji wasiopungua saba na kuwajeruhi wengine 11 katika mapambano yaliyotokea Jumanne dhidi ya kundi la Al-Shabaab huko Janale, kusini ya Somalia.

    Habari nyingine zinasema jeshi la Somalia limewaua wapiganaji wasiopungua 14 akiwemo kamanda mmoja mwandamizi wa kundi hilo katika operesheni iliyofanyika katika eneo la kusini nchini humo.

    Kundi la kiislamu la Al-Shabaab limekuwa likipambana na serikali ya Somalia kwa miaka kadhaa na kufanya mashambulizi mbalimbali nchini humo. Vikosi vya AMISOM vinalisaidia jeshi la serikali ya Somalia kupambana na kundi hilo.

    Na nchini kenya watu zaidi ya 6 wameuawa na mwingine mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab kushambulia eneo moja la kaunti ya Mandera kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia.

    Kamishna wa kaunti ya Mandera Bw Fredrick Shisia amesema, wamethibitisha vifo vya watu 6 na wengine 13 wameokolewa. Wapiganaji walitumia guruneti kuvunja mlango kabla ya kufyatua risasi dhidi ya watu waliokuwa wamelala na baadaye kukimbia.

    Bw Shisia amesema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu shambulizi hilo


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako