• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 1-Oktoba 7)

    (GMT+08:00) 2016-10-08 17:18:59

    Wanajeshi wanaomtii Machar nchini DRC kurudi nyumbani

    Naibu waziri wa habari wa Sudan Kusini Bw. Paul Akol Kordit amesema, wanajeshi 750 wa Sudan Kusini walio nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ambao ni wafuasi wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo Bw. Riek Machar, wanakaribishwa kurudi Juba.

    Jumanne wiki hii serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliomba vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuwaondoa wanajeshi hao nchini ndani ya wiki moja.

    Wapiganaji hao waliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kuhifadhiwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa, baada ya mapambano kati ya vikosi vya Bw. Machar na vya rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kulipuka mwezi Julai.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako