• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 1-Oktoba 7)

    (GMT+08:00) 2016-10-08 17:18:59

    Jeshi la Syria lakamata kilele cha mlima muhimu huko Aleppo

    Shirika la habari la taifa la Syria SANA limesema wiki hii kwamba jeshi la Syria limekamata tena kilele cha mlima cha kimkakati, na kuweza kuangalia kutoka juu sehemu zinazokaliwa na waasi mashariki mwa mji wa Aleppo.

    Hii ni sehemu ya mashambulizi yanayofanywa na jeshi la serikali hivi karibuni ili kuwafurusha waasi kutoka mji huo.

    Kwa mujibu wa shirika hilo, udhibiti wa mlima wa Sheikh Saeed unaliwezesha jeshi la Syria kuziangalia kutoka juu maeneo ya Amiriyeh na Sukariyeh zinazodhibitiwa na waasi katika kiwanda cha saruji.

    Hatua hiyo ni ushindi mpya uliopatikana katika operesheni za jeshi la Syria mjini Aleppo, ikiwa sehemu ya mashambulizi yakuwatimua waasi kutoka sehemu ya mashariki ya Aleppo wanayoidhibiti.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako