• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Novemba-17 Novemba)

  (GMT+08:00) 2017-11-17 17:10:15

  Jeshi lamzuilia rais wa Zimbabwe nyumbani

  Jeshi nchini Zimbabwe linamzuilia Rais Robert Mugabe kwake nyumbani katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

  Bw Mugabe alimwambia mwezake wa AfrikaZuma kwa njia ya simu kwamba yuko salama lakini mke wake Grace Mugabe inadaiwa amekimbilia nchini Namibia.

  Wiki hii mkuu wa majeshi wa Zimbabwe Constantino Chiwenga ameongoza wanajeshi kutwaa uongozi wan chi hiyo kwa kile alichokitaja kuwa ni kuondoa watu wenye nia mbaya kwenye chama tawala cha ZANU-PF.

  Akisisitiza utii kwa Rais Mugabe Bw Chiwenga amesema baadhi ya watu wanaopinga mapinduzi wanataka kuhujumu juhudi za mapinduzi na kuifanya Zimbabwe iwe nchi ya ukoloni mamboleo.

  Hadi wakati tukienda hewani wanajeshi walikuwa wanashika doria katika barabara za mji mkuu Harare baada ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa katika kile walichosema ni juhudi za kuwaandama wahalifu.

  Watu nchini Zimbabwe wanasubiri kuona hatua ambazo jeshi litachukua baada ya kutwaa madaraka ya nchi hiyo.

  Hatua za kijeshi zilifuatia kufutwa kwa Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye ni hasimu mkubwa wa Bi Grace Mugabe. Muungano wa Umoja wa Afrika umesema.Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kuchukua madaraka na kumzuilia Rais Robert Mugabe, inaonekana kama mapinduzi wa kijeshi,

  Mwenye kiti wa Umoja huo, Alpha Conde, alisema kuwa AU inataka kurejea mara moja hali ya kawaida.

  Jeshi linakana kufanya mapinduzi ya kijeshi, na kusema kuwa Mugabe yuko salama, na kuwa hatua zao ni dhidi ya waalifu wanaomzunguka.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako