• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Novemba-17 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-17 17:10:15
     

    Australia yapiga kura kwa wingi kuhalalisha ndoa za jinsia moja

    Watu nchini Australia wamepiga kura kwa wingi wiki hii katika hatua ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja kwenye kura hiyo ya kihistoria.

    Kura ilionyesha kuwa asilimia 61.6 ya watu walipiga kura kuruhuru wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa.

    Wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wamekuwa wakisherehekea maeneo ya umma wakiimba na kucheza.

    Waziri mkuu Malcolm Turnbul alisema serikali yake kwa sasa itaruhusu kupitishwa sheria hizo bungeni ifikapo krismasi.

    Matokeo hayo ya Jumatano yanafikisha kikomo iliyokuwa wakati mmoja kampeni kali.

    Kura hiyo yenyewe imekosolewa na wale wanaounga mkono ndo za jinsia moja wengine wakisema kuwa haikuhitajika wakati bunge lilikuwa na uwezo wa kuijadili moja kwa moja.

    Watu walikuwa wanashiriki kwa hiari kinyume na uchaguzi ambao ni wa lazima nchini Australia.

    Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ambai ni wapiga kura walishiriki katika zoezi hilo la majuma 8 ambapo swali moja tu liliulizwa, "sheria ya ndoa inaweza kubadilishwa kuruhusu wapenzi wa jinsia moja kufunga ndo?"


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako