• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Novemba-17 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-17 17:10:15

    Marekani yaongoza mashambulizi ya anga dhidi ya Kundi la IS na Al-Shabaab Somalia

    Jeshi la Marekani wiki hii limethibitisha kuwa limefanya mashambulizi mawili dhidi ya Kundi la IS na Al-Shabaab mapema jana nchini Somalia na kuwaua magaidi kadhaa.

    Kituo kikuu cha kijeshi cha Marekani barani Afrika AFRICOM kimesema shambulizi la kwanza dhidi ya Kundi la Al-Shabaab lilifanyika saa tisa hivi alfajiri katika eneo la Lower Shabelle, umbali wa kilomita 64 magharibi mwa mji wa Mogadishu. Na shambulizi la pili dhidi ya Kundi la ISIS lilifanyika saa tatu mchana katika eneo la Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia.

    AFRICOM imeongeza kuwa vikosi vyake vitaendelea kuchukua hatua zote halali kwa kushirikiana na tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, na vikosi vya usalama la Somalia SNSF, ili kupunguza matishio ya ugaidi na kuwalinda wananchi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako