• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Novemba-17 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-17 17:10:15

    Watu 11 wafariki katika ajali ya ndege kwenye hifadhi ya Ngorongoro Tanzania

    Watu 11 wamefariki dunia baada ya ndege waliokuwa wakisafiria aina ya Cessna Caravan ya kampuni ya Coastal Aviation kuanguka kwenye eneo la volkano ya Empakaai, katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania.

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Bw Charles Mkumbo amethibitisha kuwa watu hao 11 waliondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha jana asubuhi, wakielekea kwenye mbuga ya wanyamapori ya Serengeti, ikiwa na rubani mmoja na abiria kumi.

    Ofisa habari wa eneo la Ngorongoro Bw Nickson Nyange amesema waokoaji wamepelekwa kwenye eneo la ajali, lakini hadi sasa bado wanaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo.

    Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa ndege inayomilika na shirika hili kukumbwa na ajali.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako