• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Novemba-17 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-17 17:10:15

    Mahakama kuu ya Kenya kusikiliza mashauri matatu ya pingamizi la uchaguzi wa urais

    Mahakama kuu ya Kenya wiki hii imeanza kusikiliza mashauri matatu ya pingamizi kuhusu uchaguzi wa urais, miezi mitatu baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8 kufutwa.

    Uchaguzi uliorudiwa Oktoba 26 umepingwa na aliyekuwa naibu waziri Bw. Harun Mwau na wanaharakati wa haki za binadamu Bw. Njonjo Mue na Khelef Khalifa.

    Pingamizi hilo linasema upigaji kura uliorudiwa ni batili, kwa kuwa tume huru ya uchaguzi ya Kenya IEBC ilishindwa kuwafanya wagombea wapitie upya kwenye mchujo baada ya upigaji kura wa awali kufutwa.

    Pingamizi lingine lililotolewa na Shirika la IDG linalowataka viongozi wa chama cha upinzani cha NASA kuwajibika na mabavu na vurugu zilizotokea katika uchaguzi.

    Mahakama hiyo itakuwa na siku sita kusikiliza na kufanya uamuzi, na siku ya mwisho ya kutoa hukumu itakuwa Novemba 20.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako