• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

    Serikali ya Sudan Kusini yatarajia kufikia makubaliano ya mwisho ya amani na kundi la waasi

    Mazungumzo kati ya serikali na kundi la waasi nchini Sudan Kusini kuhusu masuala yaliyobaki ya makubaliano ya kusimamisha mapambano na kugawanya madaraka yaliyosainiwa hivi karibuni yamepiga hatua, na kutarajiwa kufikia mwafaka wa mwisho.

    Hayo yamesemwa wiki hii na msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Bw. Michael Makuei Lueth. Amesema mazungumzo kuhusu makubaliano ya mwisho ya amani kuhusu masuala ya utawala wa sehemu, idadi ya majimbo, na nyongeza ya wizara tano yanaendelea vizuri mjini Khartoum nchini Sudan.

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, mpinzani wake Bw. Riek Machar pamoja na makundi mengine kadhaa ya upinzani tarehe 5 walifikia makubaliano mapya ya kugawana madaraka na kusimamisha mapambano. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Bw. Machar atarejeshewa cheo chake cha makamu wa kwanza wa rais, na vyeo vingine vinne vya makamu wa rais vitagawanywa kwa serikali na makundi ya upinzani.

    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako