• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

  (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

  Boubacar Keïta achaguliwa kwa kura 67.17% Mali

  Rais anayemaliza muda wake nchini Mali Ibrahim Boubacar Keïta ("IBK") ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais kwa 67.17% ya kura. Mpinzani wake Soumaïla Cissé amepata 32.83% ya kura. Kiwango cha ushiriki kilifikia 34.54%, kulingana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii.

  Matokeo hayo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 12 yametangazwa na Waziri wa Utawala wa Mali Mohamed Ag Erlaf kwenye radio na televisheni ya taifa. Rais Ibrahim Boubacar Keita ("IBK") ambaye alikua madarakani kwa miaka mitano amechaguliwa ten akuliongoza taifa hilo linalokabiliwa na mdororo wa kiusalama.

  Ibrahim Boubacar Keita, maarufu "IBK", ndiye mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyotangazwa na Waziri wa Utawala. Huu ni ushindi mkubwa kwa sababu amepata 67.17% ya kura. Mpinzani wake, kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé, amepata 32.83% ya kura.

  Rais anayemaliza muda wake alipewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya duru ya pili ya uchaguzi. Alishinda kwa karibu asilimia 42 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Julai 31 wakati ambapo alipambana na wagombea wengine 24.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako