• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

  (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

  Rais wa Somalia abadilisha maofisa waandamizi wa usalama

  Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia amefanya mabadiliko makubwa duru za usalama na ofisi yake, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama nchini humo.

  Rais Farmajo amewateua Jenerali Dahir Aden Elmi kuwa kiongozi mpya wa vikosi vya ulinzi, luteni kanali Odawaa Yusuf Rageh kuwa naibu mkuu wa majeshi, na Hassan Nur Ol-u-jog kuwa kamanda wa jeshi la majini la Somalia.

  Bw. Hussein Amhed na Bw. Said Ahmed Kadiye wameteuliwa kwa manaibu makamanda wa kikosi cha polisi.

  Mabadiliko hayo yamekuja wakati Somalia ikiungwa mkono wa AMISOM, inaimarisha operesheni zake za kuwaondoa wapiganaji wa Al-Shabaab kutoka ngome zao nchini humo.

  Na wakti huo huo Vikosi vya Somalia na Tume ya kulinda amani ya Umoja wa mataifa nchini humo AMISOM vimezindua operesheni za kijeshi kwenye eneo la Lower Shabelle, kwa lengo la kuwaondoa magaidi wa kundi la Al-Shabaab.

  Mkuu wa jeshi la Somalia Bw. Adbiweli Jama Hussein amesema operesheni hiyo inalenga kuwasaka wapiganaji waliokimbilia kaskazini.

  Bw. Hussein pia ameviagiza vikosi vya serikali ya Somalia kuimarisha ushirikiano na AMISOM na washirika wengine kwenye operesheni dhidi ya Al-Shabaab.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako