• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

  (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

  Meli ya uokoaji yawasili Malta ikiwa na wahamiaji 141

  Meli ya uokoaji wa kibinadamu MV Aquarius imewasili katika bandari ya Malta ilikuwa na wahamiaji 141 waliookolewa. Kabla ya kupewa ruhusa ya kuingia kwenye bandari ya Malta, meli hiyo ilikuwa imekwama baharini kwa muda wa siku nne, baada ya nchi za Mediterranean ikiwa ni pamoja na Malta, Italia, Hispania na Tunisia kukataa kuipokea meli hiyo.

  Wahamiaji kwenye meli hiyo walikuwa ni pamoja na watoto 73 waliokolewa kwenye meli mbili za mbao zilizokuwa zinajaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kutoka Libya.

  Serikali ya Malta imesema baada ya wakimbizi hao kufanyiwa vipimo vya kimatibabu, watapelekwa katika kituo cha kupokea wahamiaji, na baadaye watagawanywa kwa Ufaransa, Ujerumani, Luxembourg, Ureno na Hispania.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako