• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

  (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

  Ethiopia yajenga vituo vya matibabu ya dharura kwa ajili ya raia wake wanaorudi kutoka Djibouti

  Ethiopia imejenga vituo vya matibabu ya dharura ili kutoa huduma za afya kwa ajili ya raia wake wanaorudi kutoka Djibouti.

  Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Amir Aman amesema vituo vinne vya matibabu ya dharura vimeanzishwa katika sehemu ya Dire Dawa na sehemu nyingine jirani, ili kutoa matibabu ya lazima kwa Waethiopia waliorudi kutoka Djibouti kutokana na vurugu za kimabavu. Ameongeza kuwa hadi sasa watu 74 wamepata matibabu, na kati yao 24 wamepata nafuu.

  Zaidi ya wahamiaji elfu 30 wa Ethiopia nchini Djibouti wamepoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya kulipiza kisasi, baada ya vurugu zilizotokea wiki iliyopita nchini Ethiopia, ambazo zilisababisha vifo vya watu wasiopungua 10, na kati yao watano ni Wadjibouti.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako