• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 11-Agosti 17)

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:06:16

    Uganda yakanusha habari kuhusu kutokea kwa homa ya Ebola

    Shirika la Afya duniani WHO limesema watu watatu waliodhaniwa kuambukizwa virusi vya Ebola mashariki mwa Uganda, wamethibitika kuwa hawajaambukizwa ugonjwa huo baada ya kupimwa.

    Shirika hilo limesema watu wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walioripotiwa kuambukizwa na virusi vya Ebola katika sehemu ya mpaka ya Kasese, wamethibitishwa kuwa hawana virusi hivyo, huku mtu wa tatu ambaye ni mwanamke mjamzito alifariki kwa kutokwa na damu kabla ya kujifungua pia vipimo vimethibitisha kuwa sio virusi vya Ebola.

    Mwakilishi wa WHO nchini Uganda Bw. Yonas Tegegn Woldemariam, ameliambia Shirika la habari la China Xinhua, kuwa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Uganda, lakini tishio la ugonjwa huo ni halisi.

    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako