• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 1-Desemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-12-07 19:03:41

  Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara waachiliwa huru

  Mahakama mjini kigali, Rwanda imetangaza kwamba mwanasiasa Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara hawana hatia na kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.

  Mahakama imesema kwamba imefanya uamizi huo kutokana na kwamba upande wa mashitaka haukutoa ushahidi wa kutosha.

  Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

  Muendesha mashtaka alikuwa ameomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela.

  Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa.

  Waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini.

  Kadhalika Diane Rwigara na Mamake walishitakiwa kuchochea chuki na kusambaza uvumi kwa lengo la kuhamasisha umma kugoma dhidi ya utawala.

  Uamuzi huo wa wiki hii ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na gamu baada ya Diane Rwigara na mamake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hii wakiwa hawako kizuizini.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako