• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 1-Desemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-12-07 19:03:41

  Polisi Ethiopia wakamata watuhumiwa wanaohusika na vurugu za hivi karibuni

  Polisi nchini Ethiopia wamewakamata maofisa watano waandamizi wa serikali ya jimbo wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika eneo le Benishangul Gumuz, magharibi mwa Ethiopia.

  Maofisa hao waliwekwa kizuizini kwa tuhuma za kuchochea migogoro miwili mjini Assosa mwezi Juni, pamoja na mapambano yaliyotokea hivi karibuni kwenye maeneo ya mpakani katika majimbo ya Oromia na Benishangul Gumuz mwezi Novemba.

  Wakitangaza kukamatwa kwa maofisa hao, polisi wa Ethiopia pia wamesema wataimarisha juhudi zao ili kuwafikisha wahusika wote wa vurugu hizo mbele ya sheria.

  Imefahamika kuwa watu zaidi ya kumi waliuawa kwenye mapambano ya kikabila yaliyotokea mjini Assosa na maeneo ya karibu mwezi Septemba mwaka huu.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako