• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 1-Desemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-12-07 19:03:41

  Ndege mbili za jeshi la Marekani zagongana Japan

  Ndege mbili za jeshi la Marekani zimegongana nchini Japan na kutumbukia baharini.

  Kumekuwa na oparesheni kubwa ya uokoaji kuwatafuta wanajeshi watatu wa Marekani.

  Ndege hizo zilikuwa na wanajeshi saba.

  Wanajeshi wawili waliokolewa. Mmoja wao yuko hali nzuri kwa mujibu wa wa wizara ya ulinzi nchini Japan. Hali ya mwanajeshi mwingine haikujilikana mara moja.

  Ndege hizo zilikuwa za KC-130 na F/A-18 kutoka kambi ya Iwakuni karibu na Hiroshima.

  Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndege hizo zilianguka wakati wa kuongezwa mafuta zikiwa angani.

  Jeshi la wanamaji halijathibitisha rasmi hilo likitaja kisa hicho kuw hitilafu.

  Kulikuwa na wanajeshi watano kwenye ndege ya C-130 na wawili kwenye ndege ya F-18. Mmoja wa wale waliookolewa alikuwa kwenye ndege ya kijeshi, kwa mujibu wa maafisa wa Japan.

  Taarifa kwennye mtandao wa Facebook iliyochapiswa na kikosi cha wanamaji ilisema ajali hiyo ilitokea umbali wa kilomita 320 ktoka pwani.

  Ndege za Marekani zilikuwa zimepaa kutoka kambi ya Iwakuni na zilikuwa kwenye mazoezi ya kawaida wakati hitilafu hiyo ilitokea.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako