• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 1-Desemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-12-07 19:03:41

  Wakimbizi 193 wa Nigeria nchini Libya warudishwa makwao kwa hiari

  Shirika la kimataifa la wakimbizi IOM imesema, wahamiaji haramu 193 wa Nigeria wamerudishwa nyumbani kwa hiari kutoka Libya.

  Taarifa iliyotolewa na IOM imesema, kutokana na msaada wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya, wakimbizi hao wamerudishwa makwao salama. Hivi sasa, kambi za wakimbizi nchini Libya zimejaa maelfu ya wahamiaji haramu waliookolewa au kukamatwa na kikosi cha usalama cha Libya.

  Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pia limesema, wakimbizi 133 wakiwemo wanawake na watoto wamehamishwa kutoka Libya hadi Niger.

  Libya imekuwa ni sehemu inayovutia wahamiaji haramu wanaotaka kuvuka bahari ya Mediterranean na kuingia barani Ulaya, kutokana na nchi hiyo kuwa na hali ya machafuko tangu mwaka 2011 ilipokumbwa na vurugu

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako