• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 1-Desemba 7)

  (GMT+08:00) 2018-12-07 19:03:41

  Uganda yataka kushirikiana na DRC kupambana na Ebola

  Uganda iko katika hali ya tahadhari kubwa kutokana na uwezekano wa kuenea kwa ugonjwa wa Ebola kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, na inataka kushirikiana na nchi hiyo kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

  Wizara ya afya ya Uganda imesema, hivi karibuni serikali ya DRC ilizuia familia tano zenye wagonjwa wa Ebola waliotaka kuvuka mpaka kuingia nchini Uganda, jambo linaloifanya nchi hiyo kuwa na wasiwasi kuwa ugonjwa huo hatari unaweza kuenea nje ya DRC.

  Waziri wa wizara hiyo Ruth Aceng ameongoza ujumbe wa Uganda kwenda nchini DRC ambako wanajadiliana hatua za kuchukua kwa pamoja ili kupambana na ugonjwa huo.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako