• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 25-Mei 31)

    (GMT+08:00) 2019-05-31 18:04:40
     

    Utekelezaji wa mkataba wa soko huria la Afrika waanza

    Mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika hatimaye umeanza kufanya kazi Alhamisi ya wiki hii, hatua ambayo umoja wa Afrika unasema una imani kuwa utapanua zaidi soko la bara la Afrika lenye watu bilioni 1.2.

    Umoja wa Afrika unasema hatua hii italifanya bara la Afrika kufanya biashara za wenyewe kwa wenyewe zitakazofikia thamani ya dola za Marekani trilioni 2.5.

    Mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika umeridhiwa na nchi 22 mwezi April mwaka huu, idadi ambayo ndio ilikuwa ikihitajika ili kuufanya uanze kufanya kazi, imesema taarifa ya umoja wa Afrika.

    Makubaliano ya kuanza kazi kwa awamu ya kwanza yanatarajiwa kuzinduliwa Julai 7 wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi nchini Niger.

    Hatua hii inafikiwa wakati ambapo bado kuna mataifa kadhaa hayajatia saini kuridhia mkataba huu, wakitaka kwanza baadhi ya masuala kupatiwa ufumbuzi, ikiwemo kuboreshwa kwa miundo mbinu, mapambano ya rushwa na kutambua asili ya bidhaa.

    Nchi 52 kati ya 55 ambazo ni wanachama wa umoja wa Afrika wametia saini kuazishwa kwa ukanda wa eneo la biashara huria tangu mwezi Machi mwaka 2018 huku Nigeria.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako