• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 25-Mei 31)

    (GMT+08:00) 2019-05-31 18:04:40

    Rais wa Nigeria aapishwa kwa muhula wa pili

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameapishwa kwa muhula wa pili wa miaka minne.

    Rais Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo walikula kiapo Jumatano kwenye uwanja wa Eagle ulioko katikati ya mji mkuu, Abuja.

    Kaimu mwanasheria mkuu wa Nigeria Tanko Muhammad alisimamia kiapo cha rais, kikifuatiwa na kushushwa na kupandishwa kwa bendera ya taifa na ya ulinzi, na kupigwa mizinga ya heshima mara 21.

    Hakuna viongozi wa nchi za nje waliohudhuria halfa hiyo. Wageni waliohudhuria ni pamoja na viongozi wa usalama, mabalozi, na viongozi wa mahakama na wafanyabiashara wakubwa.

    Buhari aliapishwa kwa mara ya kwanza kuwa rais wa Nigeria Mei 29 mwaka 2015, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa mgombea wa upinzani kuchukua madaraka kutoka kwa rais aliyekuwepo madarakani.

    Na huko kanda ya Kusini mwa Afrika Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa kwa muhula wake wa pili ambao pia ni wa mwisho, huku akitoa wito kwa taifa kushikamana ili kutimiza matarajio ya nchi hiyo.

    Bw. Mutharika amewataka washindani wake kukubali ushindi wake kwa sababu kutakuwa na mshindi mmoja tu, huku akiwashukuru wananchi wa Malawi kwa kumpigia kura na kuongeza kuwa ushindi wake ni wa watu, utawala wa sheria na demokrasia.

    Bw. Mutharika alishinda uchaguzi kwa kupata asilimia 38.57 ya kura zote, huku mshindani wake mkuu Bw. Lazarus Chakwera kutoka kundi kuu la upinzani MCP akipata asilimia 35.41 ya kura zote.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako