• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 28-Oktoba 4)

  (GMT+08:00) 2019-10-04 16:54:53

  Marekani yafungua tena ubalozi wake nchini Somalia

  Hatua hii ya Marekani kufungua tena ubalozi wake Mogadishu ni ishara tosha na kubwa, karibu miongo mitatu baada ya ubalozi huo, ulioko katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa, kufungwa.

  Serikali imesema hii ni hatua mpya kuelekea kurudi kwa uhusiano kati ya Somalia na Marekani.

  Mnamo tarehe 5 Januari 1991, wakati Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, watu 281 walihamishwa kutoka ubalozi wa Marekani hadi kwenye chombo cha jeshi la Marekani kilokuwa kimepiga kambi kwenye pwani ya Mogadishu.

  Imechukua miaka 28 kwa Marekani kufungua tena uwakilishi wao katika mji mkuu, wa Somalia, Mogadishu. Kitendo chenye ishara kubwa, kuonyesha jinsi gani usalama umeimarika nchini Somalia na nchi hizi mbili kuanza tena ushirikiano mpya.

  Wakati huo huo, Washington ilitambua serikali ya Somalia mnamo mwaka 2013, miaka miwili baada wanamgambo wa Kiislamu, Al Shabab, kuondoka katika mji wa Mogadishu.

  Hatua hii ya kufunguliwa tena kwa ubalozi wa Marekani nchini Somalia inakuja miaka mitano baada ya uteuzi wa balozi.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako