• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 28-Oktoba 4)

    (GMT+08:00) 2019-10-04 16:54:53

    Nabil Karoui asalia jela

    Mahakama ya Rufaa nchini Tunisia imefutilia mbali ombi la kuachiliwa huru Nabil Karoui lililotolewa na mawakili wake.

    Nabil Karoui amefuzu katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais imepangwa kufanyika Oktoba 13 mwaka huu.

    Nabil Karoui, ambaye ni mfanyabiashara maarifu nchini Tunisia, ameshitakiwa tangu mwaka 2017 kwa utakatishaji fedha na ukwepaji kodi.

    Nabil Karoui hatashiriki katika kampeni ya uchaguzi wa wabunge. Wafuasi wake, pamoja na mkewe, Salwa Smaoui, wataendelea kunadi sera yake katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo, kama walivyofanya tangu mapema mwezi Septemba.

    Kuna swali moja ambalo bado halijawekwa wazi: lile la kushiriki kwa mfanyabiashara huyo katika mijadala ya televisheni na mpinzani wake Kaïs Saeid kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

    Uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa pia unaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Nabil Karoui iwapo atashinda uchaguzi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako