• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 28-Oktoba 4)

  (GMT+08:00) 2019-10-04 16:54:53

  Tanzania yasema bado haijawasilisha vipimo vya Ebola WHO

  Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amethibitisha kuwa nchi yake haikuwapatia Shirika la Afya Duniani (WHO) sampuli za vipimo vya wagonjwa wawili walioshukiwa kuwa na virusi vya Ebola, kwa kuwa vipimo vya ndani vilithibitisha kuwa watu hao hawakuwa na ugonjwa huo.

  Mwishoni mwa Mwezi Septemba, WHO ilitoa taarifa ambayo iliilaumu Tanzania kwa kutokutoa ushirikiano juu ya uchunguzi wa wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na dalili zinazofanana na za Ebola.

  Chini ya kanuni za Afya za kimataifa, makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama, nchi zinalazimika kuiarifu WHO mara tu zitakapokuwa na milipuko ya magonjwa makubwa ya kuambukiza ambayo yanaweza kuwa hatari kwa majirani zao na ulimwengu.

  Waziri Mwalimu amesisitiza kuwa Tanzania haina uwezo wa kuficha ugonjwa wa Ebola.

  Bi Mwalimu anasema taarifa zinazoenezwa dhidi ya Tanzania zinaifanya serikali kuamini kuwa kuna njama za makusudi za kuichafua nchi hiyo zinazofanywa kwa makusudi.

  Tayari nchi za Marekani na Uingereza zimeshatoa angalizo kwa raia wake wanaopanga kuzuru Tanzania kuchukua tahadhari juu ya tishio la maambukizi.

  Mlipuko wa Ebola unaendelea kushika kasi Mashariki mwa nchi jirani ya Tanzania ya DRC na tayari zaidi ya watu 2,000 wamepoteza Maisha toka mwaka 2018.

  Wakati huo huo Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kuwepo kwa juhudi za kuvuka mpaka kati ya nchi wanachama ili kuwa tayari kukabiliana na changamoto ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

  Umoja wa Afrika kupitia kituo cha kuzuia na kupambana na magonjwa (Africa CDC) umesema kwenye jarida lake kuwa, ushirikiano kwenye kujiandaa na mwitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola kwa nchi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi jirani, kutasaidia kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako