• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 28-Oktoba 4)

    (GMT+08:00) 2019-10-04 16:54:53

    China yaadhimisha miak 70 ya jamuhri

    China imefanya maadhimisho makubwa ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

    Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na gwaride kubwa la jeshi na umma limefanyika katika Uwanja wa Tian'anmen, katikati ya mji wa Beijing.

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti, rais na katibu mkuu wa Kamati kuu ya kijeshi ya China Xi Jinping, ametoa hotuba muhimu na kukagua gwaride la jeshi.

    Amesisitiza kuwa katika miaka 70 iliyopita, kutokana na kuwa na imani ya pamoja na jitihada za pamoja, watu wa China wamepata mafanikio makubwa yanayong'ara kote duniani.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China imesimama kideteimara katika mashariki mwa ulimwengu, na hakuna nguvu yoyote inayoweza kuyumbisha hadhi ya China, na kuwazuia watu wa China na taifa la China kupiga hatua mbele.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema kuwa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China miaka 70 iliyopita, kulibadilisha kikamilifu hatma ya China iliyokuwa maskini, dhaifu na kunyanyaswa, na kufungua njia ya kuelekea ustawi mpya wa taifa la China.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) na Kikosi cha Askari Polisi cha Watu wa China (CAPF) wanatakiwa kulinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, na kulinda kithabiti amani ya dunia. Ametoa wito kwa wananchi wote wa China kushikamana zaidikwa karibu, ili kutimiza Ustawi Mpya wa Taifa la China.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako