• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36
     

    WHO yasema ugonjwa wa Ebola sasa umedhibitiwa vijijini nchini DRC

    Mkurugenzi mtendaji wa idara ya dharura za kiafya wa shirika la afya duniani WHO Dr. Michael Ryan, amesema juhudi za kuondoa virusi vya Ebola nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kong DRC zinaonekana kuwa na mafanikio.

    Akizungumza mjini Geneva kuhusu hali ya ugonjwa huo kwa sasa, Dr. Ryan amesema virusi vya ugonjwa huo sasa vimedhibitiwa katika maeneo ya vijijini vilikogunduliwa mwezi Agosti mwaka jana, na huu ni wakati wa kutokomeza virusi hivyo.

    Amesema kwa sasa virusi vya ugonjwa huo viko katika eneo la pembe tatu kati ya Mambasa, Kimanda, Beni na Mandima, eneo ambalo lipo katikati ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

    Amesema changamoto kubwa kwa sasa ni kuwa baadhi ya maeneo hayo yanafikika baada ya kusafiri kwa pikipiki kwa muda wa saa tano, na makundi kadhaa yenye silaha yanaendelea na shughuli zake katika maeneo hayo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako