• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36
     

    Baraza la utawala la Sudan lateua jaji mkuu na mwanasheria mkuu

    Baraza la utawala nchini Sudan limetangaza uamuzi wa kuwateua jaji mkuu na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa imesema Bibi Nemat Khair ameteuliwa kuwa jaji mkuu, na Bw. Taj Al Hebr ameteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Msemaji wa baraza hilo Bw. Mohamed Suleiman, amesema uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa waraka wa katiba uliowasilishwa kwenye wizara ya sheria na kuchapishwa kwenye gazeti la kiserikali.

    Bw. Suleiman amesema baada ya jaji mkuu na mwanasheria mkuu kuchukua nafasi zao, wataanza kazi ya kuchagua mkuu wa baraza la mahakama.

    Bibi Khair ni mwanamke wa kwanza kuwa na wadhifa huo nchini Sudan.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako