• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    Rais Magufuli wa Tanzania asema fedha zitakazorudishwa kutoka wahalifu wa kiuchumi zitatumika kujenga mitandao ya barabara

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesema pesa zitakazorudishwa kutoka kwa wahalifu wa kiuchumi zitatumika kujenga mitandao ya barabara nchini humo.

    Akiongea baada ya kuzindua barabara mpya ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa kilomita 76.6 mkoani Katavi, rais Magufuli amesema baada ya kuunganisha maeneo yote kwa mtandao wa barabara, itakuwa rahisi zaidi kuiunganisha nchi hiyo na nchi jirani zake.

    Septemba 22, rais Magufuli alimpa siku saba Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) Bw. Biswalo Mganga kutafakari namna ya kutoa msamaha kwa watu walioshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi au utakakishaji fedha ambao watarudisha fedha walizotakakisha.

    Septemba 30 Bw. Mganga amesema watu 467 walioshtakiwa kwa uhalifu wa kifedha nchini humo wamewasilisha maombi ya kutafuta msamaha wa rais.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako