• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    UNICEF yatoa chanjo milioni 1.6 za kipindupindu Sudan

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limekabidhi chanjo milioni 1.6 za kipindupindu kwa Sudan ili kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo.

    Msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephen Dujarric amesema chanjo hiyo imefika kwa wakati muhimu ambapo watu wanaoambukizwa ugonjwa huo wanazidi kuongezeka. UNICEF imekodi ndege maalum iliyofikisha chanjo hiyo.

    Wizara ya afya ya Sudan imetangaza kuwa watu nane wamefariki dunia katika majimbo ya Blue Nile na Senner tangu ugonjwa huo utokee mwezi mmoja uliopita.

    Chanjo hiyo imefadhiliwa na Shirikisho la chanjo duniani, ambalo limesema pia linashirikiana na wadau wengine kuimarisha mifumo ya kusafisha maji, kusambaza bidhaa za kusafisha maji na kutoa msaada mwingine wa kiufundi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako