• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    Idadi ya vifo yafikia 104 kwenye maandamano nchini Iraq

    Idadi ya watu waliouawa kwenye maandamano yaliyotokea Baghdad na miji mingine ya Iraq imeongezeka na kufikia 104, huku watu zaidi ya elfu 6 wakijeruhiwa wakiwemo walinzi usalama wengi. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Saad Maan amesema watu wasiojulikana wenye silaha walishambulia ofisi za vyombo vya habari vya ndani na nje, na uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo unaendelea.

    Rais Barham Salih wa Iraq amewataka waandamanaji nchini humo kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili watu wafahamishwe kuhusu hatua za mageuzi. Rais Salih pia amehimiza kuzuia maandamano kuzidi kuwa makubwa ili kuepusha watu kutoka nje kuingilia mazungumzo ya kitaifa. Pia amesema vitendo vya kuwashambulia watu wanaoandamana kwa amani na askari wa usalama, na vya kuvilenga vyombo vya habari na wafanyakazi wake, havikubaliki nchini Iraq. Amesema Iraq inatakiwa kuwa nchi ya kidemokrasia, ambapo haki na uhuru vinaheshimwa na katiba inafuatwa.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako