• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    Mtoto wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini akana tuhuma dhidi yake

    Mtoto wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefikishwa mbele ya Tume ya Zondo nchini humo ambapo alikana tuhuma zote juu yake.

    Duduzane Zuma ameiambia Tume hiyo kuwa, familia ya Gupta haikuwepo katika mkutano ambao inadaiwa kuwa aliyekuwa naibu wa wizara ya fedha nchini humo Mcebisi Jonas alipewa hongo ya dola za kimarekani milioni 39.7 ili awe waziri wa wizara hiyo.

    Mwezi Agosti mwaka jana, Jonas aliweka wazi mbele ya Tume hiyo kuwa alikutana na Duduzane katika hoteli ya Hyatt Oktoba 23 mwaka 2015, na kwamba mkutano wao baadaye ulihamishiwa nyumbani kwa familia ya Gupta ambapo alipewa hongo hiyo na nafasi ya uwaziri.

    Familia ya Gupta imetoa taarifa ikikana kufanyika kwa mkutano huo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako