• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 5-Oktoba 11)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 17:15:36

    Operesheni ya Uturuki yasababisha watu 70,000 kukimbia makazi kaskazini mwa Syria

    Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu nchini Syria limesema operesheni ya kijeshi ya Uturuki dhidi ya vikosi vya Kikurdi kaskazini mwa Syria imesababisha watu elfu 70 kukimbia makazi yao.

    Shirika hilo lenye makao makuu nchini Uingereza limesema vijiji 11 vimeingia mikononi mwa vikosi hivyo na waasi washirika wa Syria, na hadi sasa raia 10 wameuawa.

    Shirika la habari la Syria SANA limesema Uturuki imefanya mashambulizi makali ya mizinga dhidi ya miundombinu ikiwemo vituo vya maji, mitambo ya kuzalisha umeme, visima vya mafuta na makazi ya watu katika mikoa ya Hasakah na Raqqa, nchini Syria.

    Wizara ya ulinzi wa Uturuki wiki hii imesema jeshi lake limefanya opresheni ya kijeshi ya ardhini dhidi ya Kundi la Wakrudi huko kaskazini mwa Syria.

    Shirika la Habari la Syria limesema, raia wanane wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Uturuki kwenye maeneo ya mkoa wa Hasakah, kaskazini mashariki mwa Syria, ikiwa ni pamoja na mji wa Qamishli, al-Darbasiyah, na Ras al-Ayn.

    Akizungumzia shambulizi hilo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inaona siku zote kwamba mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Syria lazima uheshimiwe na kulindwa.

    Amesema Jumuiya ya kimataifa na pande zote husika zinapaswa kujitahidi kuweka mazingira mazuri katika kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa suala la Syria, na kuepusha hali ya sasa ya Syria kuwa mbaya zaidi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako