Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mwongozaji wa michezo ya kuigiza televisheni, mkulima Zhou Yuanqiang
  •  2006/06/05
    Zhou Yuanqiang ni mmoja wa wakulima milioni 900 wa China. Miaka 13 iliyopita aliongoza wakulima wenzake kuhariri na kutengeneza mchezo wa kuigiza televisheni kwa kamera yake ya video.
  • Mhifadhi wa utamaduni wa jadi wa China Bw. Feng Jicai
  •  2006/05/15
    Bw. Feng Jicai ni mwandishi wa vitabu na mchoraji mashuhuri nchini China. Katika miaka ya karibuni, kwa moyo wote anajishughulisha na kazi ya kuokoa na kuhifadhi utamaduni wa jadi unaokaribia kutoweka na ameanzisha "mradi wa kuhifadhi utamaduni wa jadi wa China". Juhudi zake zinaungwa mkono na sekta mbalimbali za jamii, watu wanamsifu kuwa ni "mhifadhi wa utamaduni wa jadi wa China".
  • Mwimbaji mashuhuri Li Shuangjiang
  •  2006/04/10
    Bw. Li Shuangjiang alizaliwa mwaka 1939 mjini Harbin, kaskazini mashariki mwa China. Alipokuwa katika shule ya msingi mara nyingi alipata tuzo katika maonesho ya michezo ya sanaa ya miji na mikoa.
  • Bw. Guo Degang na mchezo wake wa ngonjera ya kuchekesha
  •  2006/03/20
    Ngonjera ya kuchekesha iliwahi kuwa ni aina moja ya michezo ya sanaa inayowavutia sana Wachina, lakini katika miaka ya karibuni mchezo wa aina hiyo umekuwa katika hali ya kudidimia, baadhi ya watu walitoa kauli wakisema, "Tuokoe mchezo wa ngonjera ya kuchekesha!"
  • Mwigizaji nyota wa filamu Liu Xiaoqing
  •  2006/03/06
    Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, Bi. Liu Xiaoqing alikuwa mwigizaji maarufu sana nchini China kutokana na uigizaji wake hodari. Lakini wakati huo alipokuwa kileleni katika uigizaji wake ghafla aliacha uchezaji wa filamu akaanza kufanya biashara, na biashara yake ilikuwa mbaya hata alitiwa gerezani kutokana na kukwepa kulipa kodi kubwa
  • Mwongozaji wa michezo ya TV Zhang Jizhong
  •  2005/12/05
    Bw. Zhang Jizhong anajulikana sana kwenye fani ya michezo ya TV kwa wote kwani michezo yake mingi inawavutia sana watizamaji.
  • Mwendeshaji Tamthilia wa Kisasa Zhang Guangtian
  •  2005/10/25
    Bw. Zhang Guangtian ni mtu anayezungumzwa sana katika nyanja ya tamthilia, watu wanaomwunga mkono wanaona kuwa, yeye ni mtangulizi wa mageuzi ya tamthilia, na watu wanaompinga wanaona kuwa yeye si mtaalamu wa tamthilia hata kidogo.
  • Mkutubi mkuu wa maktaba ya taifa ya China, Bw. Zhan Furui
  •  2005/08/29
    Mkutubi mkuu wa maktaba ya taifa ya China Bw. Zhan Furui ni mtaalamu wa utafiti wa mshairi mkubwa Li Bai wa Enzi ya Tang (618-907). Alisema, moyo wa mshairi Li Bai ambao mtu lazima atoe mchango hata akiwa kabwera kabisa, unamhimiza siku zote katika kazi yake ya utafiti na usimamizi wa shughuli za maktaba.
  • Mwandishi chipukizi Wang Xiaoli
  •  2005/07/11
    Vitabu vya safari ya utalii au vitabu vya kueleza mandhari, mila na desturi katika nchi za ng'ambo havikosi kupatikana katika maduka ya vitabu, ingawa vitabu hivyo havionekani sana ndani ya vitabu chungu nzima.
  • Mchoraji mashuhuri Bi. Zhang Fuying kisiwani Taiwan
  •  2005/05/09
    Siku hizi maonesho ya picha za mchoraji mkubwa Bi. Zhang Fuying anayetoka kisiwani Taiwan yanafanyika katika jumba la makumbusho la taifa mjini Beijing.
  • Msanii mashuhuri wa ngojela za kuchekesha, Hou Yuewen
  •  2005/04/27
    Ngojela za kuchekesha ni moja ya aina michezo ya sanaa za jadi nchini China, ambayo hadi leo imekuwa na historia ya karibu miaka mia mbili. Hapo awali sanaa hiyo ilikuwa ni mazungumzo na simulizi miongoni mwa raia. Mchezo huo unachekesha kwa maneno, kuiga vitendo na kuimba kwa lengo la kudhihaki hali mbaya iliyotokea katika jamii au kuchekesha kwa hadithi za ajabu.
  • Msanii mashuhuri wa ngojela za kuchekesha, Hou Yuewen
  •  2005/03/11
    Ngojela za kuchekesha ni moja ya aina michezo ya sanaa za jadi nchini China, ambayo hadi leo imekuwa na historia ya karibu miaka mia mbili. Hapo awali sanaa hiyo ilikuwa ni mazungumzo na simulizi miongoni mwa raia. Mchezo huo unachekesha kwa maneno, kuiga vitendo na kuimba kwa lengo la kudhihaki hali mbaya iliyotokea katika jamii au kuchekesha kwa hadithi za ajabu.
  • Msomi mkubwa wa China Bw. Feng Yidai
  •  2005/03/10
    Mnamo tarehe 23, katika sikukuu ya taa ya Kichina, Wachina wanapojumuika na jamaa zao kusherehekea siku hiyo kama ilivyo desturi yao, msomi na mfasiri mkubwa wa China Bw. Feng Yidai alifariki dunia mjini Beijing kutokana na ugonjwa.
  • Mwimbaji wa Tibet Ronzonrja
  •  2005/02/28

    Katika miaka ya karibuni waimbaji wengi chipukizi wa makabila madogo madogo wameibuka nchini China, mmoja kati yao ni Ronzonrka. Neno "Jiuzhaigou" ni jina la mahali mkoani Sichuan nchini China. Huko kuna vijiji tisa vya Watibet, ni mahali penye mandhari ya kupendeza kimaumbile. Wimbo huo kwa sauti na maneno uliisifu mandhari ya maskani ya mwimbaji huyo.

  • Mwimbaji Mashuhuri wa Nyimbo za Kikabila Rozi Amuti
  •  2005/01/24
    Siku moja katika majira ya baridi, tulimtembelea mwimbaji Rozi Amuti nyumbani kwake mjini Beijing. Tulikaribishwa kwa ukarimu, tulikuwa tukisikiliza kanda ya nyimbo alizoimba za kabila lake la Uygur huku tukiburudika kwa chai ya maziwa, tulijihisi kama tuko katika sehemu ya mbali mkoani Xinjiang, magharibi kabisa mwa China.
    1 2 3 4