Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-24 15:55:32    
Tangazo 0524

cri

Kwanza tunapenda kuwaarifu wasikilizaji wetu kuwa, Naibu spika wa bunge la umma la China Bwana Xu Jialu tarehe 18 katika Jumba la mikutano ya umma la Beijing alikutana na wasikilizaji wa Radio China kimataifa waliochaguliwa kuwa washindi katika chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya, na kuwapa tuzo.

Bwana Xu Jialu aliwapongeza wasikilizaji washindi na kuwafahamishia historia, utamaduni na hali ilivyo ya sasa ya maendeleo ya China pamoja na mustakbali wake. Hasa aliwafahamisha wazo la falsafa ya wananchi wa China la kufuatilia amani na utulivu tangu enzi na dahari, pamoja na nia imara ya wananchi wa China ya kutimiza muungano wa taifa.

Radio China kimataifa imepokea majibu karibu laki 5 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 140 kuhusu chemsha bongo juu ya ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya. Wasikilizaji 11 kutoka Kenya, Albania, Australia, Marekani, Pakistan, Sri Lanka, India, Laos, Uturuki, Tunisia na Brazil wamechaguliwa kuwa washindi maalum ambao wamepata nafasi ya kutembelea mijini Beijing na Xian, China, miongoni mwao yupo msikilizaji wetu Xavier Telly Wambwa wa Bungoma, Kenya.

Msikilizaji wetu Bwana Wambwa amekuja Beijing, China usiku wa tarehe 16 Mei. Siku ya pili baada ya kuja Beijing, alitembelea Hekalu la Tangzesi, alifurahia sana kuliona hekalu hilo. Alisema:

Nachukua nafasi hii kwanza kumshukuru mwenyezi mungu aliyeumba mbingu na dunia na kila kitu kiliomo. Namshukuru kwa kuiwezesha kusafiri salama salimini hadi hapa nchini China.

Kwanza kabisa pokeeni salamu kutoka kwa wasikilizaji wenzangu wa CRI nchini Kenya na Bara la Afrika kwa ujumla.

Kwa majina ni Bw. Xavier L Telly Wambwa na nilizaliwa mwaka wa 1972 katika kijiji cha Nalondo, wilaya ya Bungoma, mkoani magharibi nchini Kenya.

Safari hii ni mara ya kwanza kwa Bwana Wambwa kutembelea China, hata ni mara ya kwanza kwake kutoka nje ya nchi yake Kenya. Alipofika Beijing, aliona Beijing, China ni tofauti na ile aliyokuwa akiitarajia.

Bwana Wambwa amefurahia kuchaguliwa kuwa mshindi maalum wa kupata nafasi ya kutembelea China, anasema siku za baadaye ataendelea kusikiliza vizuri vipindi vya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa, na kutoa mchango mkubwa zaidi ya kuongeza maelewano na urafiki kati ya Radio China kimataifa na wasikilizaji wake.

Wakati wa kuchagua washindi, idhaa yetu ya kiswahili kwa kweli ilifanya juhudi kubwa kuhakikisha msikilizaji wetu mmoja anachagulia. Kazi haikuwa rahisi, kwani Radio China kimataifa ina idhaa 38 za lugha za kigeni, na kila idhaa inatarajia msikilizaji wake atachaguliwa kuwa mshindi, hivyo kila mwaka tunaweza kusema kuwa, idhaa zote zinafaya juhudi za kugombea nafasi hii kwa ajili ya wasikilizaji wake, si rahisi kuipata nafasi hiyo. Ni matumaini yetu kuwa, wasikilizaji wetu wataendelea kusikiliza vipindi vyetu, siku za usoni bado kuna nafasi, tutaendelea kufanya chini juu ili kuwapatia wasikilizaji wetu nafasi, waliofanya bidii tunawaomba waendelee na juhudi, ili kutupa nguvu ya kuweza kuwapigania. Tunatumani kuwa huenda watapata nafasi muda si mrefu ujao, subira yavuta heri.

Picha Husika >>

Idhaa ya kiswahili 2005-05-24