Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-27 16:27:59    
Mto unaopendeza waunganisha vivutio vyote vya mkoa wa Guangxi

cri

Mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang la Guangxi una mandhari nzuri na vivutio vingi vya utalii, ambapo watu wa makabila madogo mbalimbali wanaishi huko, kila kabila lina mvuto wake kipekee. Kama mnapenda kujua mengi zaidi kuhusu mkoa huo, karibuni msikilize kipindi maalum cha chemsha bongo kuhusu ujuzi wa vivutio vya utalii mkoani Guangxi, ambapo tutatangaza makala 5 maalum zitakazowajulisha hali mbalimbali ya mkoa huo.

Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka iliyopita, kila baada ya kusoma makala moja, tutauliza maswali mawili. Baadaye kamati yetu ya uthibitishaji itachagua wasikilizaji washindi wa nafasi ya kwanza, pili na tatu pamoja na nafasi maalum. Washindi watakaopata nafasi za kwanza, pili na tatu watapewa kadi ya kumbukumbu na zawadi; na wasikilizaji washindi watakaopata nafasi maalum wataalikwa kuja China na kutembelea mkoa wa Guangxi nchini China. Na kuanzia tarehe 20 mwezi huu tutaanza kusoma makala ya kwanza ya mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa vivutio vya utalii mkoani Guangxi, China, karibuni mtusikilize, na tunawakaribisha wasikilizaji mshiriki kwenye chemsha bongo ya mwaka huu.

Na leo tunawaletea makala ya kwanza ya chemsha bongo kuhusu "Mto unaopendeza unaouganisha vivutio vyote vya mkoa wa Guangxi, China". Kabla ya kuanza kusoma makala hii ya kwanza, tunatoa maswali mawili: 1. Alama ya utalii ya mji wa Guilin ni nini? 2. Urefu wa jumla wa Mto Lijiang ni kilomita ngapi? Tafadhali sikilizeni kwa makini ili muweze kupata majibu kutoka kwa makala tunayowasomea.

Watalii wengi kutoka nchi za nje waliokuja China kwa utalii walisema, tukitaka kutazama mabaki ya kale ya utamaduni tutakwenda kwenye mji wa Xian, na tukitaka kutazama mandhari nzuri ya milima na mito tutakwenda mjini Guilin. Mji wa Guilin unajulikana nchini na nje kwa milima yake ya kijani, mto wenye maji safi na mapango ya milimani yenye maajabu. Kiini cha sehemu ya vivutio vya utalii ya Mto Lijiang kiko mjini Guilin, kuanzia kwenye wilaya ya Xing'an ya kaskazini hadi wilaya ya Yangshuo ya kusini, sehemu hiyo inaungamana kwa Mto Lijiang. Kwenye sehemu hiyo kuna vivutio vingi vya utalii kama vile Mto Lijiang, Pango la mawe Ludi, Pango la mawe Qixing, Kilele cha Duxiu, Mlima Fobo na Mlima Diecai, na kati ya hiyo Mlima Xiangbi unaweza kuwakilisha umaalum wa Mji wa Guilin.

Mlima Xiangbi uliosimama kidete kando ya Mto Lijiang ni alama ya Mji wa Guilin, huu ni mlima maarufu sana mjini Guilin, mlima huo umeumbwa kwa mawe ya chokaa yaliyolundikana chini ya bahari zaidi ya miaka milioni 300, umbo la mlima huo linafanana sana na tembo mkubwa aliyenyoosha pua mkonga wake na kuvuta maji ya mto, na katikati ya mkonga wa tembo na kwenye mwili wa tembo kuna tundu moja mviringo, maji ya mto yanapita kwenye tundu hilo. Kila ifikapo siku yenye mbalamwezi, ukitazama Mlima Xiangbi kutoka mbali unaweza kuona kuwa kwenye tundu hilo mviringo ni kama kuna mbalamwezi unaoelea juu ya maji, na kivuli cha mbalamwezi wa angani kwenye mto kinaonesha kama kuna mbalamwezi mwingine kwenye mto, hii ni hali ya ajabu inayowavutia watu. Bw. Ma Weimin anayeishi chini ya Mlima Xiangbi alituelezea hadithi kuhusu Mlima Xiangbi, akisema:

"Hekaya ya zama za kale nchini China ilisimulia kuwa, tembo wengi wa mfalme wa mbinguni Yuhuang walipofika kwenye Mji wa Guilin waliona mandhari ya Milima na Mto wa mji huo ni nzuri sana, wakang'ang'ania huko na hawakutaka kuondoka. Mfalme wa mbinguni Yuhuang alitoa agizo mara kwa mara la kuwataka tembo warudi mbinguni, lakini tembo mmoja kati yao alikataa katakata, kwani hakutaka kuondoka kutoka kwenye Mji wa Guilin wenye mandhari nzuri. Mfalme Yuhuang alikasirika sana, akachukua panga na kumwua tembo huyo, panga hilo lilimpiga tembo huyo na kumtundika kwenye kando ya Mto Lijiang, tembo huyo akabaki daima mjini Guilin.

Watalii wanaotembelea mjini Guilin huvutiwa sana na mandhari nzuri ya milima na mto wa mji huo, baadhi yao wanatembea kwenye kando ya mto, wengine wanakaa kwenye mikahawa ya chai kunywa chai na kupiga soga, wengine wanakaa kimya kwenye kando ya mto kuvua samaki, wote hao wanaonekana kuwa na raha mustarehe.

Katika sehemu nyingi duniani, kadiri shughuli za utalii zinavyoendelezwa na idadi ya watalii inavyongezeka, ndivyo kunakuwa na shinikizo kubwa kwa uhifadhi wa mazingira ya kila sehemu, hata kusababisha uharibifu kwa mazingira. Lakini watalii wanaotembea mjini Guilin wanaona hewa ya huko siku zote ni safi sana, na maji ya Mto Lijiang siku zote ni safi sana hata vitu vya ndani ya maji vinaonekana wazi. Kuhusu hayo ofisa wa idara ya utalii ya Mji wa Guilin Bw. Chen Yunchun alisema, ili kuhifadhi vizuri mazingira ya asili ya Guilin, wameweka kanuni ya kuhifadhi kwanza mazingira wakati wa kuendeleza shughuli za utalii, na kazi ya kuendeleza shughuli za utalii lazima ifanyike kwenye msingi wa kuhifadhi mazingira ya asili. Alisema:

"Kazi ya uhifadhi wa mazingira ni ya kwanza, miradi ile ambayo haiwezi kupita ukaguzi wa kiwango cha uhifadhi wa mazingira haiwezi kukubaliwa. Hivi sasa mjini Guilin, kwanza viwanda vinavyotoa moshi haviruhusiwi kuendelezwa, pili viwanda vinavyotoa uchafuzi kwa mazingira haviruhusiwi kuendelezwa, ni lazima kuendeleza viwanda vya sayansi na teknolojia za hali ya juu".

Baada ya kutembelea Guilin, watalii wengi wanaweza kuelekea kwenye wilaya ya Yangshuo kutoka Mto Lijiang. Kwani sehemu ya Yangshuo ina mandhari nzuri zaidi kuliko Guilin. Chanzo cha Mto Lijiang kiko kwenye Mlima Maoer, kaskazini mwa Guilin, na urefu wa Mto Lijiang ni zaidi ya kilomita 400. Kuna umbali wa kilomita 83 kati ya Mji wa Guilin na Wilaya ya Yangshuo, mandhari ya kando mbili za mto zinapendeza sana, sehemu hiyo ni sehemu kubwa zaidi duniani ya milima yenye mapango ya chokaa na mto wenye mandhari nzuri kabisa. Kwenye kando mbili za Mto Lijiang, vilele vyenye maumbo ya ajabu vinasimama kidete, misitu minene, miamba inayostawi, mashamba na vijiji vinaonekana popote pale. Mtalii kutoka Ujerumani Bw. Hermawa Haerthe alisema, akipanda mashua na kutembea kwenye Mto Lijiang, mandhari nzuri ya njiani inamvutia na kumfurahisha sana. Alisema:

"Kabla ya kutembelea Mto Lijiang niliwahi kuona picha nyingi kuhusu mandhari ya mto huo, lakini naona hali halisi ya mto huo niliyoshuhudia inapendeza kweli. Naona mandhari ya sehemu hiyo ni kama picha nzuri. Katika maskani yangu pia kuna sehemu yenye mandhari nzuri kama hiyo, ingawa sehemu hiyo siyo kubwa lakini mandhari yake ni nzuri ya kushangaza watu".

Kwenye Mto Lijiang, Mlima Huashan ni maarufu zaidi, vivuli vya Huangbu kwenye mto ni vivutio vizuri zaidi. Mlima Huanshan una urefu wa zaidi ya mita 400, kwenye miamba ya mlima huo inayokaribia mto kuna kanda zenye rangi mbalimbali zilizoumbika kutokana na majani ya mtoni yaliyokufa na kuwa vitu vya chokaa. Rangi hizo za kiviumbe na rangi asili ya madini ndani ya mawe "zimechora" picha za maumbile za "farasi" na "samaki" wenye maumbo mbalimbali. Chini ya anga buluu na mawingu meupe, vivuli hivyo vilivyoko karibu na kando ya mto vimeumbwa kuwa mandhari ya ajabu ya "meli inayotembea juu ya mlima".


1 2