Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-27 16:27:59    
Mto unaopendeza waunganisha vivutio vyote vya mkoa wa Guangxi

cri

Kwenye Wilaya ya Yangshuo, kila ifikapo usiku, Mto Lijiang wa sehemu hiyo huwa inakuwa kama ni jukwaa la michezo ya Sanaa, ambapo mchezo wa nyimbo na ngoma wa "Liu Shanjie kwenye kumbukumbu halisi" unaoneshwa kwenye sehemu ya mto yenye urefu wa kilomita 2 wilayani Yangshuo. Chini ya giza totoro, sauti ya wimbo wa kienyeji inasikika kutoka mbali, kwa ghafla taa zinawaka, na milima iliyoko kando ya upande mwingine ikaonekana ghafla mbele ya watu, hali ambayo inawashangaza watu na kupigiwa makofi mara kwa mara.

Maonesho hayo ya michezo ya Sanaa yanawashirikisha wachezaji zaidi ya 600, lakini wengi kati yao siyo wasanii maalum, bali ni wakulima wa sehemu hiyo. Katika maonesho ya dakika 70, wasanii hao wanaonesha maisha ya kawaida ya wavuvi wanaoishi kwenye kando mbili za Mto Lijiang na desturi na mila za watu wa makabila madogo madogo wanaoishi kwenye sehemu hiyo, shughuli za kuvua samaki, kilimo, kufuga ng'ombe na hekaya na nyimbo kienyeji za kabila la wazhuang yote hayo yameoneshwa vilivyo pamoja na mandhari nzuri ya mto na milima.

Bw. Thomas Laubis na mkewe kutoka Ujerumani walisifu sana maonesho hayo. Wao walifika China kwa mara ya kwanza kutalii, mwanzoni walipanga kukaa kwa wikiendi moja tu, lakini sasa wanataka kung'ang'ania kukaa huko kwa muda mrefu zaidi. Bw. Thomas alisema:

"Sehemu hiyo ina mandhari nzuri kweli, safari hii hakika siyo safari ya mwisho kwa sisi kuja China au Barani Asia".

Baada ya kutazama maonesho ya nyimbo na ngoma ya "Liu Shanjie kwenye kumbukumbu halisi", watalii wengi wanapenda kukaa kwa usiku huo wilayani Yangshuo. Wilaya ya Yangshuo si kama tu ina mandhari nzuri zaidi kuliko Mji wa Guilin, bali pia kuna mtaa mmoja wa kale unaowavutia zaidi watalii. Mtaa huo wa magharibi una urefu wa zaidi ya mita 500 tu, lakini historia yake imekuwa na zaidi ya miaka 1400. Kwenye mtaa huo uliotandikwa kwa matofali ya mawe ya kijani, nyumba zilizojengwa zamani sana kwa matofali ya kijani na yenye mapaa ya rangi ya kijani zinawavutia watalii wengi wa nchi za nje kwa mvuto wao wa kiasili.

Kwenye mtaa wa magharibi, popote unapokwenda unaweza kuona watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambao baadhi yao wanatembeatembea kwenye njia ya mawe, wengine wanatazama vitu vya kale kwenye maduka, wengine wanang'ang'ania kwenye maduka ya michoro na vitabu. Kwenye mkahawa unaoitwa Jufulou, mwendeshaji wa mkahawa huo Bw. Lu Huaping alikuwa anawafundisha watalii wengi kutoka nchi za nje kupika kitoweo cha kichina. Bw. Lu alisema, semina anayoandaa kwenye mkahawa huo kuhusu kupiga vitoweo vya kichina inakaribishwa na wageni wengi, kila siku watalii zaidi ya 10 wanaweza kuja kushiriki kwenye semina yake na kujifunza kupika kitoweo cha kichina kutoka kwake. Alisema:

"Mwanzoni nilianzisha baa, marafiki wengi wa nchi za nje walikuja kwenye baa yangu, na wengi kati yao walipenda sana kwenda jikoni kwetu kutazama tunavyopika vitoweo vya kichina, na wapishi wetu wakipata nafasi, wageni hao walikuwa wanakwenda jikoni kujifunza upishi kutoka kwa wapishi hao. Baadaye nilianzisha mkahawa, hivyo nikaandaa semina ya kujifunza mapishi ya kichina kwenye mkahawa huo".

Kwenye mtaa wa magharibi si kama tu kuna mikahawa kama mkahawa huo wa Bw. Lu, bali pia kuna mikahawa mingi ya mapishi ya nchi za magharibi, mikahawa ya kahawa na baa, na mikahawa hiyo kweli ni yenye "harufu nzito ya Kimataifa", hata chapa za mikahawa hiyo na vitoweo vyake vimeandikwa kwa maandishi ya Kiingereza, kifaransa na kijerumani. Na waendeshaji wengi wa mikahawa hiyo ni wageni, kwa mfano Bw. Alf Young wa Baa inayoitwa Kichwa cha Ng'ombe.

Bw. Alf Young ni m-australia, alipokuja China kutalii miaka mitano iliyopita alivutiwa na mandhari nzuri ya mtaa wa magharibi, aliishi kwenye sehemu hiyo yenye mandhari nzuri na hali ya utulivu. Baadaye alioana na mkazi wa huko na wakapata mtoto, na kuanzisha baa hiyo inayoitwa Kichwa cha ng'ombe. Bw. Alf Young alisema, anataka kuishi kwenye mtaa wa magharibi huko Yangshuo kwa maisha yake yote. Alisema:

"mimi nimeishi hapa kwa miaka mitano, naipenda sana sehemu hii, mtaa wa magharibi pia ni wenye mtindo wa nchi za magharibi, ukiishi hapa unaweza kupata marafiki wengi na kupiga soga nao. Na sehemu ya Yangshuo ni yenye mandhari nzuri sana, unaweza kutembea barabarani, pia unaweza kupanda baiskeli hapa, na katika majira ya siku za joto unaweza kuogelea mtoni, hivyo nimeamua kuishi hapa. Mimi nilifahamiana na mke wangu hapa na tukapendana, sasa tumekuwa na mtoto. Maisha yangu ya siku za mbele yako kwenye mtaa wa magharibi.

Sasa tunarudia maswali yetu mawili ya leo: 1. Alama ya utalii ya mji wa Guilin ni nini? 2. Urefu wa jumla wa Mto Lijiang ni kilomita ngapi?


1 2