Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Mito ya Masikio
  •  2005/01/15
        Mito ya masikio imepata jina hilo kwa sababu sehemu yake ya katikati hubonyea ndani ili masikio ya mtu anayeutumia yasikandamizwe anapoulalia. Mito hiyo hushonwa kwa kitambaa cha pamba na kutiwa nakshi za tarizi huko Wilaya ya Qingyang, Jimbo la Gansu. Kuna aina nyingi za nakshi, na zinazoonekana kistadi.
  • Ukuta wa Sanaa ya Michongo ya Mawe
  •  2005/01/07
        Deyang ni mji mpya ulioko kwenye sehemu ya magharibi ya Jimbo la Sichuan. Mji huu ni safi sana na una msingi imara wa viwanda na mandhari nyingi za kiutamadimi. Kati ya mandhari hizo, Ukuta Wenye Sanaa ya Michongo ya Mawe ya Deyang ndio unaowavutia zaidi watalii kwa mtindo wake wa kipekee wa ujenzi na kiwango cha juu cha sanaa.
  • Liu Kunyan na michoro ya Ndani ya Chupa
  •  2004/12/24
        Michoro ya ndani ni michoro iliyochorwa upande wa ndani wa kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga. Liu Kunyuan mwenye umri wa miaka 41 ni mwanachama pekee na mkulima wa Jumuia ya Kimataifa ya Kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga ya China. Michoro aliyochora ndani ya kichupa cha kuwekea tumbaku ya unga inajulikana sana katika sanaa hiyo.
  • Kitambaa cha Yunjin
  •  2004/12/17
        China ni nchi iliyovumbua kufuga viwavi vya hariri na kufuma vitambaa vya hariri duniani. Katika zama za kale, "Jin" (kitambaa cha hariri kilichotiwa nakshi), kiliwakilisha kiwango cha juu, tulijua kufuma "jin" katika Enzi ya Shang. Ufumaji wa "jin" alistawi sana ilipofika Enzi ya Qing, wakati huo sehemu ya Kusini ya China ilikuwa kiini cha ufumaji wa hariri.
  • Kichwa cha Simba Bandia
  •  2004/12/10
        Wakati wa sikukuu, wakulima wa Wilaya ya Pizhou, sehemu ya kaskazini ya Jimbo la Jiangsu hucheza ngoma ya simba. Wachezaji wawili wananyanyua sanamu ya simba huku wakicheza ngoma. Sanamu hiyo ina sehemu mbili: kichwa na kiwiliwili. Shi Shengrong na mkewe ni mafundi maarufu wa kutengeneza kichwa cha simba. Ufundi wao umekuwa ukirithiwa kwa vizazi vitano, kwa hivyo utengenezaji na maumbo ya kichwa cha simba umebaki kuwa ni sanaa ya jadi. Wakati wa msimu usio na kazi za kilimo, familia nzima inajumuika katika utengenezaji wa kichwa cha simba.
  • Sanamu za ukutani
  •  2004/12/03
        Sanamu za ukutani zenye sura za wachezaji wa opera za mitindo ya aina kwa aina na zenye kuonyesha uhai zimetengenezwa kwa makopo yaliyotupwa au vizibo vya chupa za divai, na zinawastaajabisha sana watu. Sanamu hizi ni kazi ya mikono ya Lu Rongwei, kada wa Idara ya Sanaa na Michezo ya Eneo la Huangpu, mjini Shanghai.
  • Kofia za Watoto
  •  2004/12/01
        Kupata watoto ni jambo la furaha kwa familia. Katika Jimbo la Shanxi, watu hufanya sherehe mbalimbali za kutoa pongezi siku mtoto anapozaliwa, kutimiza mwezi mmoja, siku mia na mwaka mmoja. Zawadi muhimu katika sherehe hizo ni kofia zenye rangi za kupendeza, hii ni mila ya watu wa huko.
  • Sanaa Jadiia
  •  2004/10/08
    Han Zengqi ni msanii maarufu wa kufinyanga sanamu za udongo mjini Beijing. Nyumba yake ni ndogo, lakini ndani kunakaliwa na "maelfu ya askari na farasi", juu ya kitanda na meza kumejaa "wapanda farasi" waliokwishafinyangwa na kwenye ua sanamu za udongo za watu na farasi zimepangwa mstari baada ya mstari juu ya vipande vya mbao kusudi zikaushwe kwa upepo.
  • Vyombo vya Vanishi?Sanaa ya Pekee ya China
  •  2004/09/17
  • Nakshi za Shanxi
  •  2004/08/20
    1  2  3  4