Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Maua yanayotengenezwa kwa samli
  •  2005/06/24
        Maua ya samli ni sanamu zinazotengenezwa kwa samli. Samli hupatikana kutokana na maziwa mabichi ya ng'ombe na ni chakula kisichokosekana katika maisha ya kila siku ya Watibet. Wasanii wa kienyeji hutia rangi mbalimbali ndani ya samli na kutengeneza sanamu mbalimbali kama vile: mabanda ya ghorofa, milima, mito, maua, ndege, wanyama wa thamani na wa ajabu na hekaya za dini ya Kibuddha. Maua ya samli yanayotengenezwa na malama wa Hekalu la Ta'er, mkoani Qinghai ni maarufu sana.
  • Wushu ya Shaolin
  •  2005/06/17
    Wushu (mbinu za kujihami za Kichina), ambayo hujulikana kwenye nchi za Magharibi kwa jina la gongfu, imeenea duniani kote kutokana na filamu za kungu mnamo miaka ya 1960 na 1970. ingawa filamu hizo zilipendwa na kustaajabisha sana, gongfu hutiwa chumvi mno kwenye filamu hizo.
  • Masoko ya vitu vya sanaa mjini Beijing
  •  2005/05/27
    Mtaa wa utamaduni wa kale wa Liulichang mjini Beijing una historia ya miaka zaidi ya 100. Makumi ya maduka yanayouza vitu vya kale na sanaa za kila aina yanayopambwa kwa mapambo ya mitindo mbalimbali ya kale yamesambaa katika mtaa huo wenye urefu wa mita 1,000. Ukiingia kwenye duka lolote na kununua kitu chochote kinachoonekana kama cha kawaida, basi kitu hicho huenda kina historia ya karne kadhaa.
  • Mishumaa ya Shughuli Mbalimbali
  •  2005/05/13
    Ni kawaida nchini China kutumia mishumaa iliyopambwa nyakati za shughuli kama vile harusi, sherehe za kuzaliwa na mazishi. Mishumaa iliyotengenezwa kusini mwa mkoa wa Jiangsu ni maarufu sana kutokana na mabombwe yake ya kupendeza na ustadi wa kuitengeneza na mpaka sasa bado inatumiwa sana na wakulima wa huko.
  • Tiara za Weifang
  •  2005/04/22
    Tiara ambazo zinachukuliwa kama ni michezo ya starehe ya jadi na kwa ajili ya kusherehekea sikukuu, zimeenea sana kwa wakazi wa mijini na vijijini nchini China. Mwanzoni mwa majira ya mchipuko kabla na baada ya Sikukuu ya Qingming ya kila mwaka, ambapo hali ya hewa inakuwa nzuri na majani huchipua, na miti huchanua ni kipindi kizuri mno cha kurusha tiara.
  • Jumba la Muziki la Beijing
  •  2005/04/15
    Jumba la Muziki la Beijing, ambalo ni la hali ya juu kabisa nchini China kwa kutumbuiza muziki pekee, linajulikana sana kwa maonesho ya upigaji wa muziki hali ya juu. Ndani ya jumba hilo kuna mapambano ya anasa na mwangaza mwanana wa taa zinazomulika kutoka pande zote nne. Kwenye kuta za ukumbi wa mapumziko na kwenye ujia, kumetundikwa picha za wanamuziki mashuhuri. Tangu jumba hilo lilipofunguliwa mwaka 1985, baadhi ya wakati lilikuwa likistawi, na wakati mwingine huko hapa kusikiliza muziki.
  • Muziki wa kale wa Dunhuang
  •  2005/04/08
    Mwanzoni mwa karne hii, kitabu cha ajabu kiligunduliwa ndani ya pango la kuhifadhi misahafu huko Dunhuang, mkoani Gansu. Maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho yalikuwa hayasomeki vizuri, kwa hivyo, wataalamu wengi walishindwa kuelewa kilichoandikwa. Baada ya miaka 90, kutokana na juhudi za wataalamu, ilithibitishwa kwamba kitabu hiki ni cha muziki na ngoma zilizofuatana na upigaji wa kikanda cha pipa ambayo ni aina ya vinanda vya kale vya China. Kitabu hiki kilinakiliwa kwa mkono wakati wa karne ya tisa, hiki ni kitabu cha zamani duniani.
  • Sanaa ya uchongaji wa mianzi
  •  2005/03/25
    Tangu zamani, mahusiano baina ya binadamu na mianzi yalikuwa makubwa. Sanaa ya uchongaji wa mianzi ilianza kutokea katikati ya Enzi ya Ming ya karne ya 15 nchini China, na imekuwa ikiendelea kuboreshwa mpaka sasa, na katika muda huu wote wamejitokeza wasanii wengi hodari katika sanaa hiyo.
  • Tausi wa Dhahabu Yang Liping
  •  2005/02/25
        Mji wa Xi Shuang Ban Na uliopo kwenye mkoa wa Yunnan nchini China ulipewa jina la "Maskani ya Yausi". Mtu akitazama chini kutoka juu, anaweza kuona vijiji zaidi ya 10 vilivyoko kwenye kingo mbili za Mto Lancang, vikiwa vimetawanyika huko na huko kama bombwe la tausi.
  • Ngoma Katika Vyombo vya Kale
  •  2005/02/18
        Kimoja miongoni mwa vitu vilivyopata zawadi kwenye maonyesho ya vitu vya kale vinavyohusu historia ya ngoma za Kichina yaliyofanya jijini Beijing, spring 1989, ni chungu cha udongo chenye umri wa miaka 5,000 cha Zama Mpya ya Mawe. Katika ukingo wake wa ndani kuna makundi matatu ya wachezangoma watano watano walioshikana mikono waliochorwa kwenye mabombwe ya maua-mfano wa kale wa uchezaji ngoma ambao haujapata kuonekana nchini China.
    1  2  3  4