• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Mei - 3 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-03 16:36:30

  Miili ya wahamiaji yapatikana-Libya

  Huku mzozo wa wahamiaji kutoka Libya kwenda ulaya ukizidi, ajali za boti kuzama kwenye bahari pia zimeongezeka.

  Wiki hii zaidi ya wahamiaji 900 wanahofiwa kuwa wamefariki kwenye ajali tofauti kati ya Libya na Italia baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama.

  Na taarifa kutoka Libya zinasema kuwa miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji, imepatikana ikiwa imetapakaa katika mwambao wa bahari karibu na mji wa Zuwara.

  Zaidi ya miili 85 imeonekana ikiwa imetapakaa.

  Ofisa kutoka shirika la msalaba mwekundu nchini humo anasema miili hiyo inahisiwa kwamba huenda ni ya watu kutoka ukanda wa jangwa la Sahara.

  Eneo linalozunguka mji wa Zuwara ni miongoni mwa sehemu za pwani ya Libya ambazo wahamiaji huanzia safari zao kuelekea ulaya.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako