• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Mei - 3 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-03 16:36:30

    Mtu aliyepanga shambulio la chuo cha Garissa auawa

    Kiongozi wa shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ameuawa hayo ni kwa mujibu wa maafisa nchini Somalia wanasema.

    Serikali ya Kenya imesema kuwa Mohamed Kuno ndiye aliyepanga njama za shambulio hilo la mwezi Aprili 2015 ambapo takriban watu 148 waliuawa wengi wakiwa wanafunzi.

    Vikosi vya Somalia vinasema kuwa yeye ni miongoni mwa watu 16 waliouawa katika shambulio la usiku katika msafara wa magari mjini Kismayu ,mji wa Bandari uliopo kusini mwa Somalia.

    Wanne ya wale waliouawa waliripotiwa kuwa maafisa wandamizi wa wapiganaji wa al-Shabab.

    Na huku Mohamed Kuno akiuwawa Watu13 wameuwawa wiki hii baada ya al-shabaab kushambulia kwa bomu na kufyatua risasi kwenye hoteli ya Ambassador mjini Mogadishu nchini Somalia, wawili kati yao wakiwa ni wabunge.

    Watu wengine 40 wamejeruhiwa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako